Di Maria;Aweka wazi kitu pekee ambacho hakipendi kuhusu klabu ya Manchester United
TZ MZUKA
09:03
0
Winga wa Mancester United Angel di Maria anasema kwamba kuna tatizo moja pekee analo katika maisha yake ya nchini Uingereza. Huku msimu ukiwa mara zote unaanza majira ya joto,raia huyo wa Argentina ameanza kuzungumzia maisha ndani Manchester.
“Kuna baridi kubwa sana hapa na giza linaingia mapema sana kuliko Uhispania.”
Nyota huyo akaongeza: “Sina tatizo na chakula au kitu chochote-hakuna tofauti kubwa baina ya nilichokuwa nacho Uhispania na nilichonacho hapa.Tatizo langu kubwa pekee ni hali ya baridi kali."