Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » » Haya ndio majibu ya madaktari ya mtoto wa Marehemu Whitney Houston, Bobbi Kristina


TZ MZUKA 06:46 0

Madaktari wa hospitali alipolazwa aliyekuwa mtoto wa mwanamuziki wa nchini Marekani,marehemu Whitney Houston, Bobbi Kristina hawana tena matumaini ya kuokoa maisha ya binti huyo


Madaktari hao wamemuomba baba yake Bobby Brown kutoa ruhusa ya kuzima mashine inayomsaidia kupumua ikiwa na maana kwamba kukubali matokeo ya kuwa hawezi kupona,TMZ imeripoti.
Vyanzo vya familia hiyo vimeiambia TMZ kuwa maamuzi sasa yako mikononi mwa baba yake Brown, na inadaiwa kuwa hataki kufanya maamuzi hayo magumu hivi sasa anasubiri mpaka baada ya weekend.
Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa Brown bado ana matumaini kuwa binti yake anaweza kupona sababu kuna mtu wa familia yake aliwahi kutoka kwenye coma baada ya siku nane.


«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani