Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » LA LIGA; Matokeo ya Atletico Madrid na Real Madrid


TZ MZUKA 09:21 0


VINARA wa La Liga Real Madrid Leo wamechapwa Bao 4-0 na Wapinzani wao wa Jadi Atletico Madrid kwenye Dabi ya Jiji la Madrid Uwanjani Vicente Calderon kwenye Mechi ya Ligi.
Licha ya kipigo hiki, Real bado wanaongoza Ligi hiyo wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Barcelona na Timu ya 3 Atletico Madrid ambao ndio Mabingwa Watetezi wa La Liga.
Leo, wakimtumia kwa mara ya kwanza Staa wao Cristiano Ronaldo, ambae alizikosa Mechi 2 baada ya kuwa Kifungoni, walishindwa kung’ara hasa Fowadi yao ambayo pia walicheza Karim Benzema na Gareth Bale.
Lakini Real walicheza wakiwa na pengo kubwa kwa kuwakosa Pepe, James Rodriguez na Sergio Ramos, ambao ni Majeruhi, na pia Marcelo ambae amefungiwa Mechi 1 baada ya kuzoa Kadi za Njano 5.
Hadi Mapumziko Atletico Madrid walikuwa mbele kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Tiago Mendes Dakika ya 14 na Saul Niguez Dakika ya 18.
Atletico waliongeza Bao la 3 Dakika ya 67 kupitia Griezmann na Mario Mandzukic kuhitimisha kwa Bao la 4 katika Dakika ya 90.
VIKOSI:
Atletico (Mfumo 4-4-2): Moya; Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira; Tiago, Gabi, Arda, Koke; Griezmann, Mandzukic
Real Madrid (Mfumo 4-3-3): Casillas; Carvajal, Varane, Nacho, Coentrao; Khedira, Kroos, Isco; Bale, Benzema, Ronaldo.
REFA: David Fernandez Borbala

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani