Ronaldo Kupelekwa shule
TZ MZUKA
13:05
0
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa maarufu duniani baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza umri wa miaka 30 .
Mchezaji huyo wa Real Madrid hivi karibuni huenda akajikuta akitumiwa katika elimu ya chuo kikuuu baada ya chuo cha British Columbia Okanagan kuanzisha kozi ambayo itakuwa na masomo yanayomhusu nyota huyu .
Chuo hiki kitaanzisha kozi ya shahada ya juu ya Sosholojia (Sociology) ambayo itakuwa inasomwa na wanafunzi kwa muda wa miaka minne huku wanafunzi hao wakijiktia kwenye umaarufu wa nyota huyu na jinsi ambavyo anaathiri watu mbalimbali duniani na utamaduni kwa jumla .
Chuo cha Biritish Columbia Okanagan kilichoko nchini Canada kinataka kuanzisha kozi ya Cristiano Ronaldo .
Profesa Luis Aguilar ambaye ameanzisha wazo hili amesema kuwa Ronaldo ni mtu mwneye umaarufu wa kipekee na ni muhimu kwa watu kufahamu umaarufu wake unavyowagusa watu tofauti duniani .
Profesa huyo ameongeza kuwa wanafunzi hawatajifunza jinsi ambavyo mchezaji huyo anavyopiga chenga au kufunga mabao akiwa uwanjani bali watajifunza jinsi alivyo na mchango hasi au chanya kwa jamii tofauti ambazo zimejaa watu wanaomfuatilia .
Endapo kozi hii itapitishwa na kuanza kutumika rasmi Ronaldo atakuwa mchezaji wa pili wa Real Madrid na Manchester United kutumiwa kama kozi ya chuo kikuu baada ya mchezaji wa zamani wa Madrid na United David Beckham ambaye ametumika katika masomo kadhaa kwenye chuo cha Strefordshire huko Uingereza