VAN GAAL KUZOA BONASI £1M MAN UNITED IKIMALIZA 4 BORA
TZ MZUKA
13:07
0
Endapo Louis van Gaal atafanikiwa kuiingiza Manchester United kwenye 4 Bora ya Ligi Kuu England na hivyo kufuzu kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao, basi atavuna Pauni Milionin1 kama Bonasi yake.
Mara alipokabidhiwa Umeneja mwanzoni mwa Msimu huu, Van Gaal alielekezwa 4 Bora ndio lengo la chini kwa Man United na ili kumpa motisha akawekewa hiyo Bonasi.Msimu uliopita, Man United chini ya David Moyes aliefukuzwa, walimaliza Nafasi ya 7 kwenye Ligi na kukosa kucheza Ulaya na hilo limeathiri mapato yao na pia kuvuruga mwonekano wao kama moja ya Klabu kubwa Duniani.
Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 4 kwenye Ligi wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya 5 Liverpool huku Mechi zikibakia 8 Msimu kumalizika.