FULL TIME: CHELSEA 1 vs 0 MANCHESTER UNITED, UNITED WAKWAMA DARAJANI
TZ MZUKA
12:57
0
Chelsea ikiwa watashinda Mechi zao 2 zinazofuata basi wao ni Mabingwa.



Kocha Jose Mourinho

Ushindi huu umewapa Chelsea uongozi wa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Arsenal na Man United kubaki Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 11 nyuma.
Chelsea walifunga Bao lao la ushindi Dakika ya 38 kupitia Eden Hazard baada ya pasi nzuri ya kisigino ya Oscar kwenye Mechi ambayo Man United walimiliki Mpira kwa Asilimia 70 dhidi ya 30 ya Chelsea.

Katika Dakika za mwishoni Refa Mike Dean aliinyima Man United Penati baada ya Ander Herrera kuangushwa ndani ya Boksi na badala yake kumpa Kadi ya Njano.

Hazard dakika ya 38 kipindi cha kwanza aliipatia bao la kuongoza kwa kufanya 1-0 dhidi ya Manchester United. Baaada ya kupata pasi safi ya kisigino kutoka Oscar na kumfunga kipa wa Man United De Gea na mechi kwenda mapumziko Chelsea wakiongoza.

