Majibu ya DNA ya mtoto wa Nay wa Mitego yatoka
TZ MZUKA
12:13
0
Majibu ya kipimo cha DNA ambacho rapper Nay wa Mitego alisema amechukua
ili kujiridhisha iwapo mtoto aliyezaa na ex wake Siwema ni wa kwake
kweli ama lah, yametoka.
Kwa mujibu wa Nay ambaye ameachana na mama watoto wake, Siwema hivi karibuni, majibu aliyopata ni ‘mazuri’ na kwamba mtoto ni wake.
“Majibu mazuri, mtoto ni wangu lakini kwa hili lililotokea si la kawaida. Mimi nimeanza life yangu mpya najua nianzie wapi na nitaishia wapi,” amesema Nay.
“Lakini for this time sio muda muafaka wa kuwa na mwanamke, kwa sababu naona nitakuwa naishia sehemu zile zile tena. Pia mama yangu amenishauri kuwa makini kwenye kuchagua aina ya mwanamke.”