Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » FA CUP- DROO ROBO FAINALI: MABINGWA ARSENAL KUTETEA TAJI OLD TRAFFORD NA MAN UNITED


TZ MZUKA 12:07 0

DROO ya Mechi za Robo Fainali za Kombe Kongwe Duniani, FA CUP, imefanyika Usiku huu na kuendeshwa na Meneja wa England, Roy Hodgson, akisaidiwa na Brian Finney, Mtoto wa Lejendari wa England na Mchezaji wa zamani wa Preston, Sir Tom Finney, ambapo Bigi Mechi iliyoibuka ni ile ambayo huenda ikachezwa Old Trafford ikiwa Manchester United wataifunga Preston North End hii Leo kwani watakutana na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, 

Arsenal. Raundi hii ya FA CUP, ambayo itachezwa Wikiendi ya Machi 7, inazo Klabu 3 toka Madaraja ya chini, Reading na Blackburn Rovers toka Championship, na Ligi 1 ipo Bradford City wakati toka Ligi Kuu England zipo 5 ambazo ni Arsenal, 

Liverpool, Aston Villa, West Bromwich Albion na Manchester United.



 DROO KAMILI:
Liverpool v Blackburn Rovers
Bradford City v Reading
Preston North End/Man United v Arsenal
Aston Villa v West Bromwich Albion

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani