Alichokisema Selena Gomez baada ya kuachana na Justin Bieber
TZ MZUKA
10:29
0
Drama bado inaendelea! Mapenzi kati ya mastaa wawili Selena Gomez na
Justin Bieber yameendelea kuwa kivutio kwa mashabiki wao na safari hii
baada ya kuwepo na taarifa za kuachana kwao,Gomez amefunguka na kusema
licha ya kutokuwa pamoja bado anampenda Bierber.
Gomez mwenye miaka 22 alipohojiwa jana alisema kwa sasa hayupo kwenye
mahusiano na mtu na hakuna kibaya kati yake na mwimbaji huyo,ingawa
amekiri wana historia ya kuachana na kurudiana mara kwa mara kwa miaka
minne sasa.
“”Nilikua ninamuheshimu na kumpenda”…Gomez aliiambia redio NRJ ya
nchini Norway wakati alipohojiwa kuhusu wimbo wake mpya wa ujulikanao
kama ‘Hearts wants what it wants’ ambao umeonekana kama umelenga kumuhamasisha Bieber ili warudiane.