Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» »Unlabelled » LA LIGA: REAL MADRID YAFUNGA MWAKA KWA REKODI MPYA, RONALDO JUU!


TZ MZUKA 03:25 0

REAL-MADRID-PONGEZIReal Madrid Jana wamepata ushindi wao wa 20 mfululizo katika Mashindano yote huku Cristiano Ronaldo akipiga Bao 2 wakati walipoifunga Ugenini Almeria Bao 4-1 katika Mechi ya La Liga.
Real wameshinda Mechi zao zote kuanzia Septemba 13 na wapo Mechi 4 nyuma ya Rekodi ya Dunia ya kushinda Mechi 24 mfululizo iliyowekwa na Klabu ya Brazil Coritiba Mwaka 2011.
Hadi Mapumziko, Real walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za Isco na Gareth Bale
Kwenye Mechi hiyo, Kipa Iker Casillas aliokoa Penati iliyopigwa na Verza.
Kipindi cha Pili Real walipiga Bao 2 nyingine kupitia Ronaldo na kushinda Bao 4-1.
Hivi sasa Ronaldo amefunga Jumla ya Mabao 32 kati Mechi 23 na kwenye La Liga ana Bao 25 katika Mechi 14.
++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Almería1
-García Rabasco 39′
Real Madrid4
-Isco 34′
-Bale 42′
-Ronaldo 81′ & 88′
++++++++++++++++++++++++
Juzi Jumanne, Real walivunja Rekodi ya Barcelona ya kushinda Mechi 18 mfululizo walipoifunga Lugorets kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mechi hii ya La Liga na Almeria ni ya mwisho kwa Real kwa Mwaka huu kwa vile wao wanasafiri kwenda Nchini Morocco kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu yaliyoanza Desemba 10 na wao wakiwa Wawakilishi wa Ulaya kama Klabu Bingwa.
wamebeba Makombe ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Copa del Rey.
Hivi sasa Real wapo Pointi 5 mbele ya Barcelona kwenye La Liga.
VIKOSI:
Almeria (Mfumo 4-2-3-1): Ruben; Michel, Navarro, Trujillo, Velez; Teye, Verza; Mendez, Soriano, Dubarbier; Hemed
Akiba: Julian, Dos Santos, Corona, Azeez, Zongo, Mane, Wellington, Bifouma.
Real Madrid (Mfumo 4-3-3): Casillas; Carvajal, Pepe, Varane, Marcelo; Illarramendi, Kroos, Isco; Bale, Benzema, Ronaldo.
Akiba: Navas, Arbeloa, Coentrao, Medran, Nacho, Jese, Chicharito.

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani