Alex Song aachana na kuchezea timu ya Taifa
TZ MZUKA
01:35
0
Baada ya Sakata la kadi nyekundu katika mchezo wa makundi katika michuano ya Kombe la Dunia, Alex Song, kiungo wa Cameroon, hakuwahi kuitwa tena kuitumikia timu yake ya taifa. Hii ikamfanya kueendelea kutumikia katikia klabu yake na kuendelea na maisha yake ya kandanda.
Sasa ni rasmi ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Cameroon baad ya kutafakari kwa muda.
Song kwa sasa anaichezea West Ham ikiwa chini ya Big Sam, imekuwa ahueni kubwa kwa klabu hiyo baada ya uamuzi wake wa kuachana na Kandanda la nchi yake.
Song akiichezea West Ham kwa mkopo kutoka Barcelona, hakuitwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu.