Usajili wa kwanza Man United huu hapa
TZ MZUKA
11:10
0
Manchester United inatarajia kumtangaza kipa Mhispania Victor Valdez
kama usajili wake wa kwanza wa mwezi huu januari wakati dirisha dogo la
usajili likiwa wazi baada ya ya kipa huyo kufanya mazoezi na United kwa
zaidi ya miezi miwili .
Valdez alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na United ili ajiweke sawa
baada ya kupona jeraha la goti ambalo limemsumbua kwa muda mrefu tangu
alipokuwa na klabu ya Barcelona katikati ya msimu uliopita .
Valdez alikuwa kwenye mipango ya kukamilisha uhamisho kuelekea klabu
ya As Monaco kabla klabu hiyo haijafanya maamuzi mengine na kuachana
naye hali iliyomfanya akose klabu baada ya kuachana na Barcelona msimu
uliopita.

Kipa wa zamani wa Barcelona atasaini mkataba wa miezi 18 na Manchester United.
Zaidi ya De Gea idadi ya wachezaji wa Kihispania kwenye kikosi cha kwanza cha United inatarajia kufika wachezaji wanne baada ya Ander Herrera na Juan Mata ambao wamekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha United msimu huu .

Victor Valdez atakuwa kipa namba mbili wa Manchester United.