Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» »Unlabelled » FA CUP: CHELSEA, MAN CITY, SPURS, SOUTHAMPTON…MATOKEO


TZ MZUKA 10:49 0


KOMBE KONGWE kabisa Duniani, FA CUP, Leo limerudia Historia yake ya maajabu kwa kishindo kikubwa baada ya Vigogo wa Ligi Kuu England, Mabingwa Manchester City, Vinara wa Ligi hiyo, Chelsea, Tottenham na Southampton wote kutupwa nje na ‘Timu ndogo’ nyingine za Daraja la chini tena wote Vigogo hao wakiwa wanacheza Viwanja vya Nyumbani kwao.
Uwanjani Stamford Bridge, Chelsea waliongoza Bao 2-0 lakini Bradford City, inayocheza Ligi 1 ikiwa ni Madara mawili chini ya Chelsea, ilizinduka na kupiga Bao 4.
Chelsea walitangulia kwa Bao za Garry Cahill na Ramires na Stead kuipa Bao 1 Bradford kabla ya Kipindi cha Kwanza kumalizika.
Kipindi cha Pili, Bradford walipiga Bao 3 kupitia Morais, Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Halliday na Yeates.        
Huko Etihad, Mabingwa wa England, Manchester City, walipigwa Bao 2-0 na Middlesbrough inayocheza pia Daraja la chini Championship kwa Bao za Kipindi cha Pili za Bamford na Garcia Martinez.
Nao Tottenham, wakicheza kwao White Hart Lane, walipigwa Bao 2-1 na Leicester City ambao walitoka nyuma kwa Penati ya Andros Townsend ya Dakika ya 19 na wao kupiga Bao mbili katika Dakika ya 83, Mfungaji akiwa Ulloa, na Dakika ya 90 kwa Bao la Schlupp.
Southampton, Timu ambayo iko Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England, ilichapwa Bao 3-2 na Crystal Palace ambayo iko Nafasi ya 13 kwenye Ligi hiyo.
Bao za Mechi hiyo zilifungwa zote Kipindi cha Kwanza na kwa Southampton kuitia Pelle, Dakika ya 9, na Dann, aliejifunga mwenyewe Dakika ya 16 huku Palace wakifunga kupitia Chamakh, Dakika ya 11 na 39, na Yaya Sanogo, Dakika ya 21.
Katika Mechi ya kwanza kabisa hii Leo iliyochezwa Ewood Park, Wenyeji Blackburn Rovers, wanaocheza Daraja la chini la Championship, walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuibwaga Swansea City inayocheza Ligi Kuu England Bao 3-1.
Kwenye Mechi hiyo, Swansea walimaliza Mechi wakiwa Mtu 9 baada ya Sentahafu wao Kyle Bartley kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 6 kwa kumwangusha Josh King aliekuwa akienda kufunga na katika Dakika za Majeruhi Mfungaji wa Swansea, Gylfi Sigurdsson, pia kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika za Majeruhi kwa rafu mbaya.
FA CUP
RAUNDI YA 4
Ratiba/Matokeo
**Saa za Bongo
Ijumaa Januari 23
Cambridge United 0 Manchester United 0
Jumamosi Januari 24
Blackburn Rovers 3 Swansea City 1
Chelsea 2 Bradford City 4
Southampton 2 Crystal Palace 3
Derby 2 Chesterfield 0
Preston North End 1 Sheffield United 1
Birmingham City 1 West Bromwich Albion 2
Cardiff City 1 Reading 2
Tottenham Hotspur 1 Leicester City 2
Sunderland 0 Fulham 0
Manchester City 0 Middlesbrough 2
2030 Liverpool v Bolton Wanderers
Jumapili Januari 25
1700 Bristol City v West Ham
Jumatatu Januari 26
2300 Rochdale v Stoke City
1800 Aston Villa v Bournemouth
1900 Brighton & Hove Albion v Arsenal
TAREHE ZA RAUNDI:
-Raundi ya 4: 24 Januari 2015
-Raundi ya 5: 14 Februari 2015
-Raundi ya 6: 7 Machi 2015
-Nusu Fainali: 18 & 19 Aprili 2015
-Fainali: 30 Mei 2015


«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani