VILLAREAL YAMUUZA PAULISTA KWA ARSENAL, WAMCHUKUA CAMPBELL KWA MKOPO, ETO’O HUYOO SAMPDORIA
TZ MZUKA
11:14
0

Klabu ya Spain Villarreal imetangaza kuwa imefikia makubaliano ya awali na Arsenal ili kuwauzia Sentahafu wao Gabriel Paulista huku Fowadi wa Arsenal, Joel Campbell, akienda kwa Mkopo Villareal hadi mwishoni mwa Msimu.
Awali Villareal walitaka Arsenal iwalipe Pauni Milioni 15 ili kukidhi Kipengele cha Mkataba wa Paulista cha kumruhusu kuondoka kabla Mkataba wake kumalizika lakini Arsenal walikuwa tayari kutoa Pauni Milioni 10 tu.
Hata hivyo, Uhamisho huu wa Paulista huenda ukanasa kupata Kibali cha Kazi Nchini Uingereza kutokana na Beki huyo mwenye Miaka 24 kutowahi kuichezea Timu ya Taifa ya Brazil.
Samuel Eto'o afuzu upimwaji Afya huko Italia Klabuni Sampdoria
Straika wa Everton Samuel Eto'o sasa yupo hatua za mwisho kuhamia huko Italy kwenye Klabu ya Sampdoria baada ya kufuzu upimwaji Afya yake.
Eto'o, mwenye Miaka 33, alijiunga na Everton Agosti 2014 kama Mchezaji huru na kuwafungia Bao 4 hadi sasa.
Hivi sasa Sampdoria wapo Nafasi ya 5 kwenye Ligi ya Serie A wakiwa Pointi 13 nyuma ya Vinara Juventus.
Eto’o, Mchezaji wa Kimataifa wa Cameroun, aliwahi kucheza Serie A akiwa na Inter Milan baada ya kuhamia hapo Julai 2009 na kuifungia Inter Bao 25 katika Misimu yake miwili.
Msimu uliopita, Eto'o, ambae amewahi kuwa Mchezaji Bora Afrika mara 4, alifunga Bao 12 katika Mechi 35 alizoichezea Chelsea aliojiunga nao kwa Mkataba wa Mwaka mmoja akitokea Klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala.