FA CUP: HERRERA, DI MARIA WAIPELEKA MAN UNITED RAUNDI YA 4 NA MATOKEO YA MICHEZO MINGINE ILIYOMALIZIKA
TZ MZUKA
10:07
0
BAO za Ander Herera na Angel Di Maria zimewapeleka Manchester United Raundi ya 4 ya FA CUP baada ya kuichapa Timu ya mkiani mwa Daraja la chini la Ligi 1, Yeovil, Bao 2-0 huko Huish Park.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili, Meneka wa Man United alifanya mabadiliko na kuwaingiza Jonny Evans, Juan Mata na Angel Di Maria na hapo ndipo Man United wakafufuka na kushinda.
Droo ya Raundi ya 4 ya FA CUP itafanywa Jumatatu Usiku.
VIKOSI:
Yeovil: Bad, Nathan Smith, Nugent, Arthurworrey, Nana Ofori-Twumasi, Ralph (Eaves - 69 '), Edwards, Foley, Dawson, Gillett, Moore
Akiba: Berrett, Hayter, Leitch-Smith, Krysiak, Inniss, Eaves, Alex Smith.
Man United: De Gea, Smalling, McNair, Blackett, Da Silva (Mata - 45 '), Ander Herrera, Fletcher, Shaw (Evans - 45'), Rooney, Falcao (Di MarĂa - 60 '), Wilson
Akiba: Evans, Di Maria, Mata, Januzaj, Lindegaard, Anderson, Lingard.