RATIBA YA LIGI KUU UINGEREZA
TZ MZUKA
23:51
0
Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, Leo wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Mabingwa Watetezi Manchester City na watacheza Mechi hii bila ya Straika wao Diego Costa ambae amefungiwa Mechi 3.
FA, Chama cha Soka England, Jana kilitangaza Adhabu ya Kifungo cha Mechi 3 kwa Costa kwa kosa la kumtimba Mchezaji wa Liverpool, Emre Can, Jumanne iliyopita wakati wa Nusu Fainali ya Capital Oe Cup.
Adhabu hiyo itamfanya aikose Mechi ya Leo na City pamoja na zile dhidi ya Aston Villa na Everton.
Chelsea, ambao wapo Pointi 5 mbele ya Man City walio Nafasi ya Pili, huenda pia wakamkosa Kiungo wao Cesc Fabregas na Filipe Luis ambao waliumia wakati wa Mechi na Liverpool ya Capital One Cup.
City wao watamkosa Kiungo wao Yaya Toure pamoja na Mchezaji wao mpya Wilifred Bony ambao wote wako huko Nchini Equatorial Guinea kuiwakilisha Nchi yao Ivory Coast kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015.
VIKOSI VINATARAJIWA:
CHELSEA: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian, Oscar, Hazard, Drogba
Akiba: Cech, Beeney, Zouma, Aké, Christensen, Mikel, Loftus-Cheek, Fàbregas, Rémy, Brown, Solanke
MAN CITY: Hart, Zabaleta, Demichellis, Kompany, Clichy, Fernando, Fernandinho Milner, Nasri, Silva, Aguero
Akiba: Caballero, Wright, Sagna, Boyata, Lampard, Kolarov, Pozo, Dzeko, Jovetic, Mangala, Navas
Refa: Mark Clattenburg
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Saa za Bongo
Jumamosi Januari 31
15:45 Hull v Newcastle
18:00 Crystal Palace v Everton
18:00 Liverpool v West Ham
18:00 Man United v Leicester
18:00 Stoke v QPR
18:00 Sunderland v Burnley
18:00 West Brom v Tottenham
20:30 Chelsea v Man City
Jumapili Januari 18
16:30 Arsenal v Aston Villa
19:00 Southampton v Swansea