UHAMISHO WA DE GEA KWENDA MADRID UKO HAPA
TZ MZUKA
11:03
0

Ofa hiyo huenda ikawa Fedha taslimu ama ikawa kumbadilisha De Gea na Straika wao Gareth Bale aende Man United.
Ingawa inaaminika Man United haina nia ya kumuuza De Gea lakini ikiwa Real watalipa zaidi ya Pauni Milioni 50 na pengine wakakubali kumbadili na Gareth Bale ajiunge na Man United huenda dili hiyo ikapita hasa ukizingatia Man United hivi sasa wamemsaini bure Kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes, mwenye Miaka 33.
Man United walimsaini De Gea kutoka Atletico Madrid Miaka Minne iliyopita kwa Dau la Pauni Milioni 18 ambalo ni Dau la Rekodi kwa Kipa huko Uingereza.
Lakini hadi sasa Rekodi ya Dunia kwa Kipa wa Bei ghali ni ile ya Miaka 14 iliyopita wakati Juventus ilipolipa Pauni Milioni 33 kumnunua Gianluigi Buffon kutoka Parma.
Habari kutoka ndani ya Real zinadai kuwa Dili hii ya kumnunua De Gea ili amrithi Iker Casillas itafanikiwa kwani Real wana desturi ya kumnasa Mchezaji yeyote wanaemtaka kama walivyomchoropoa Cristiano Ronaldo kutoka Man United Mwaka 2009.