LIGI KUU ENGLAND: BALOTELLI AIPA USHINDI LIVERPOOL KWA BAO LAKE LA KWANZA KWENYE LIGI!
TZ MZUKA
20:36
0
BAO la kwanza kabisa kwa Mario Balotelli katika Ligi Kuu England kwa Liverpool Jana limewapa ushindi wa Bao 3-2 huko Anfield walipoifunga Tottenham Bao 3-2.
Mara mbili Liverpool waliongoza kwa Bao za Markovic na Penati ya Steven Gerrard lakini mara mbili Spurs walisawazisha kwa Bao za Harry Kane, likiwa Bao lake la 23 Msimu huu, na lile la Mousa Dembele.
Lakini katika Dakika ya 83, Mario Balotelli alieingizwa kuchukua Nafasi ya Daniel Sturridge, akamalizia Krosi ya Adam Lallana na kuipa ushindi wa Bao 3-2 Liverpool.
Huko Emirates, Arsenal waliichapa Leicester City Bao 2-1 za Laurent Koscielny na Theo Walcott za Kipindi cha Kwanza na Leicester kufunga Bao lao kupitia Andrej Kramaric.
Ushindi huo umeifanya Arsenal wachukue Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England na kuishusha Manchester United hadi Nafasi ya 5 lakini Usiku huu Man United wako kwao Old Trafford kucheza na Burnley na ushindi utawashusha Arsenal.
QPR, wakicheza Ugenini huko Stadium of Light, waliona mwanga wa nadra walipoitwanga Sunderland Bao 2-0 na kuondoa wimbi la kutoshinda Ugenini katika Mechi 11 na pia kung’oka lile eneo hatari la Timu 3 za mkiani.
Bao zote za QPR zilifungwa Kipindi cha Kwanza na Leroy Fer na Bobby Zamora.
Nao Hull City wamefuta matokeo mabaya kwao kwa kupata ushindi wa Nyumbani wa Bao 2-0 walipoifunga Aston Villa ambayo sasa inazidi kudidimia na sasa ipo kwenye Timu 3 za mkiani.
Bao za Hull City zilifungwa na Dame N'Doye na Nikica Jelavic.
Arsenal 2 Leicester 1
Hull 2 Aston Villa 0
Sunderland 0 QPR 2
Liverpool 3 Tottenham