Chris Brown aachana rasmi na msoto wa miaka 6 ya kesi ya kumpiga Rihanna, amaliza ‘probation
TZ MZUKA
10:58
0
Hatimaye probation ya Chris Brown (25) kwenye kesi yake ya kumpiga
aliyekuwa girlfriend wake wa wakati huo Rihanna imemalizika, na sasa
amemalizana kabisa na kesi hiyo ikiwa ni miaka sita na mwezi mmoja toka
atende kosa hilo mwaka 2009.
Breezy ameshare habari hiyo kupitia Twitter kwa kuandika “IM OFF PROBATION!!!!!!!! Thank the Lord!!!!!!”
Staa huyo wa hit single ya ‘Loyal’ alikuwa akikabiliwa na kesi ya
kumshambulia Rihanna Feb. 8, 2009 ambapo baada ya kukutwa na hatia
alikubali kufanya kazi za jamii ili kukwepa kwenda jela.