MATOKEO YA MACHESTER CITY VS WEST BROM YAKO HAPA
TZ MZUKA
10:38
0

Silva na Pablo Zabaleta baada ya kufunga bao bao City

Silva ndie aliyefunga bao la tatu

Silva akipongezwa baada ya kuifungia bao la tatu City.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England Man City wakiwa kwao walipata msaada mkubwa wa Refa Neil Swabrick katika Dakika ya Pili alipomtoa Mcheza wa West Brom McAuley kwa Kadi Nyekundu na City kushinda Mechi hii 3-0.

Kwenye tukio hilo alieonekana kucheza Rafu ni Dawson lakini Refa alimtoa McAuley.


Ushindi huu umewafanya City wawe nyuma ya Vinara Chelsea kwa Pointi 3 tu lakini Chelsea wana Mechi 2 mkononi.

Bao za City zilifungwa na Wilfried Bony, likiwa Bao lake la kwanza kwenye Ligi tangu ajiunge Januari, Fernando na David Silva.

Wilfried Bony dakika 27 aliipatia bao la kwanza City na kufanya 1-0 baada ya kulishwa mpira na Fernando. Dakika ya 40 Fernando aliwapatia bao la pili City na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya West Brom Albion.
Dakika ya 77 David Silva anaipatia bao la 3 City na kufanya bao kuwa 3-0.

Kadi nyekundu kwa Gareth McAuley imewafanya wacheze pungufu West Brom Alibion katika kipindi cha kwanza dakika ya 2 ikiwa ni baada ya kuangushwa chini mchezaji mpya wa City Wilfried Bony.
VIKOSI:
Manchester City XI: Zabaleta, Kompany, Mangala, Clichy, Navas, Fernando, Lampard, Silva, Bony, Aguero
West Brom XI: Myhill, Dawson, McAuley, Olsson, Lescott, Baird, Morrison, Gardner, Fletcher, Sessegnon, Berahino.