Bei Ya Tiketi Za Kushuhudia Pambano La Mayweather Vs Pacquiao.
TZ MZUKA
11:28
0
Zikiwa zimebaki siku 9 kabla ya pambano
lilopewa jina la ‘Fight of the Century’ kati ya mwanasumbwi tajiri zaidi
duniani ‘Floyd Mayweathe Jr’ ambaye ana rekodi ya kutopoteza pambano
hata moja tangu aanze kucheza mchezo huo, dhidi ya mfilipino mwenye
rekodi nzuri kabisa Manny Pacquiao kufanyika, leo hii bei ya viingilio
vya kutazama mchezo huo imetangazwa.
Unaambiwa tiketi ya bei ya chini kabisa
itakayokuwezesha kuingia MGM Grand Garden Arena itakuwa ikiuzwa kwa
$1500 ambayo ni zaidi ya millioni 2.5 ya Kitanzania.
Kwa wale vibopa ambao wa kati tiketi zao zitauzwa kwa $7500.
Tiketi hizi zitaanza kuuzwa leo usiku saa 2 kwa saa za Marekani, na kundi hili za tiketi litahusisha uuzwaji wa tiketi 1000 tu.
Wakati huo huo zimetengwa tiketi za bei
ya juu zaidi ambazo zitakuwa kwa $10,000 huku nyingine zikiuzwa kwa
$200,000 kwa watu mashuhuri wenye uwezo wao.
Pia kwa wale watakaoshindwa kulipa
viingilio hivyo, umeandaliwa mpango kuandaa sehemu itakayoingiza watu
50,000 ambao watalipa viingilio $150.