Mke wa Shetta alikataa gari alilonunuliwa na mumewe
TZ MZUKA
09:18
0
Ndoa ya Shetta bado ipo kwenye mawe! Muimbaji huyo wa ‘Shikorobo’ na mke
wake Mama Qayllah bado hawana maelewano mazuri kiasi ambacho amelikataa
gari alilonunuliwa na mumewe hivi karibuni.
Shetta amekiambia kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM kuwa Mama
Qayllah amekataa kurejea nyumbani licha ya kumletea zawadi ya gari
ambayo alimuahidi kipindi cha nyuma.
“Yeah nimemnunulia gari mpya lakini amelikataa,” alisema Shettah.
“Hili gari nilimuahidi nimtamnunulia toka zamani na lilikuwa njiani sasa
limeingia na nimelichukua wakati yeye hayupo nyumbani. Nimemwambia gari
lake lipo tayari lakini amekataa. Mama Qayllah hayupo nyumbani, mimi
kama ananisikiliza naomba arudi nyumbani.”