Mrisho Ngassa ajichora tattoo ya jina la mkewe
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa jana April 21 katika mechi dhidi ya
Stand United iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
alifunga goli moja lakini hakushangilia kwa kawaida yake ya kwenda
kwenye kona ya kibendera, bali alionekana akibusu mkono wake.
Ngassa aliongea na kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM na kueleza kwanini aliubusu mkono wake.
“Nimebusu mkono kwasabababu nimechora ‘Tattoo’ ya jina la mke wangu.
Mke wangu ndio kila kitu, ndio mshauri wangu wa kila kitu, kwahiyo
nikifunga goli lazima nimbusu,” alisema.
“Tattoo niliyochora ni jina la mke wangu kwasababu nina mapenzi ya
dhati kwake, yeye ndiye mshauri wangu, anaitwa Nish Radhia. Kuna tattoo
nyingine ambayo ni siri yangu pamoja na yeye, imechorwa kifuani.”