Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » Real Madrid na Elbar na hiki ndio kingine alichofanya Cristiano Ronaldo


TZ MZUKA 12:31 0


Ligi kuu ya Hispania imeendelea tena jioni ya leo – huku Real Madrid na Elbar wakifungua pazia la mechi za leo.
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo  ameziteka tena ‘headlines’ za vyombo vya habari baada ya leo kuiongoza timu yake kupata ushindi wa magoli 3-0.
Ronaldo alifungua akaunti yake ya magoli leo kwa mkwaju wa adhabu ndogo katika dakika ya 21 ya mchezo huo – goli la leo limemfanya Ronaldo atimize magoli 38 katika La Liga msimu huu.
 Goli hilo lilotokana na mkwaju wa adhabu ndogo ni la kwanza tangu Ronaldo alipofunga goli dhidi ya Bayern Munich katika nusu fainali ya Champions League takribani miezi 12 iliyopita.
Magoli mengine ya mchezo huo yalifungwa na Javier Hernandez Chicharito dakika ya 31 na Jesse akamalizia kazi kwa goli zuri dakika ya 83.
FC Barcelona wanaongoza ligi ya Spain wanacheza na Sevilla usiku huu.


Real Madrid: Navas, Arbeloa, Varane, Ramos (Pepe 64'), Marcelo (Nacho 65'), Modric (Borges 61'), Illarramendi, Isco, Jese, Hernandez, Ronaldo
Subs not used: Casillas, Benzema, Carvajal, Munoz Jimenez
Goals: Ronaldo 21, Hernandez 31', Jese 83'
 
Eibar: Xabier Irureta, Castellano Castro, Anibarro, Rodriguez Navas, Vila Rosello Booked, Fernandez, Garcia, Carrillo (Boateng 77'), Capa, Berjon Perez (Arruabarrena 45'), Lara Grande, Del Moral Fernandez (Piovaccari 66')
Subs not used: Ekiza, Lekic, Minero Fernandez, Jimenez Merlo
Booked: Arruabarrena, Rosello, Boateng
Ref: Alejandro Jose Hernandez 
Att: 73,965

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani