SEPP BLATTER AJIUZULU URAISI WA FIFA
TZ MZUKA
11:19
0
Raisi Sepp Blatter ,79, ametangaza kujiuzulu
nafasi yake ya Urais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Tanzania
ilikuwa kati ya nchi zinazomuunga mkono Blatter na Rais wa TFF, Jamal
Malinzi alitangaza hadharani kwamba wanamuunga mkono.
Blatter ataendelea kubaki madarakani hadi hapo Fifa itakapofanya uchaguzi mkuu mpya wa viongozi na unatarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Blatter ataendelea kubaki madarakani hadi hapo Fifa itakapofanya uchaguzi mkuu mpya wa viongozi na unatarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Blatter
alifanikiwa kumshinde Prince Ali katika uchaguzi mkuu wiki iliyopita,
ametangaza kujiuzulu.

Huku wengi
wakiwa hawatarajii baada ya Fifa kuitisha mkutano, Blatter ametangaza kuachia
ngazi mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika makao
makuu ya Fifa jijini Zurich, Uswiss.
Anaachia
ngazi baada ya uongozi wake wa miaka 17 huku Fifa ikiwa inandamwa na sakata la
rushwa la dola milioni 100.

Tayari kumekuwa na taarifa kwamba huenda kujiuzulu kwake kumekuwa shinikizo kutoka nchini Marekani.
Marekani imetumia Shirika lake la Kisasusi la FBI ambalo limekuwa likifanya uchunguzi wa sakata hilo la Fifa kukabiliwa na rushwa.
Nchi nyingine ambazo zilionekana kutomuunga mkono ni Uingereza na Ufaransa ambazo waliendelea kusisitiza kwamba alikuwa akiipendelea Afrika na Amerika Kusini. Jambo lililoonyesha kulikuwa na mpango wa nchi kadhaa za Ulaya kutaka kujitoa Fifa au kutoshiriki Kombe la Dunia.
Mtandao umekuwa mkubwa ukihusisha watu lundo na serikali ya Afrika Kusini nayo imehusishwa kwamba ilitoa mlungula kupata nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2010.