Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » LADYJay Dee;Akiri Gadner alitongoza na kuwashika makalio wanawake mbele yangu


TZ MZUKA 11:04 0


Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Judith Wambura ‘Jay Dee’ amekiri mume wake wa zamani Gadna G Habash, kuwa na mahusiano na wanawake wengi hadi wafanyakazi wa bar yake jambo ambalo lilimfanya ashindwe kuvumilia kuendelea kuwa naye.
Ikiwa ni muendelezo wa maswali mbalimbali ambayo mashabiki wake wamekuwa wakimuuliza na kujibiwa kwa njia ya mtandao amesema kuwa, haoni kama amejishushia heshima kuachana na mume wake kutokana na mume wake kutokuwa na heshima na kuwatongoza wanawake na kuwashika makalio akiwa jukwaani.
Amesema kuwa hategemei kurudiana nae kutokana na kufikiria kabla ya kufanya maamuzi na kuongeza kuwa kwa ufupi maisha yake ya ndoa yalikuwa ya misukosuko kutokana na kupigwa na mume wake kugombana na wateja wakija katika bar yake.
Ameongeza kuwa ni mapema kusema kama ataolewa tena na haimaanishi kuwa hatakuja kupenda tena na kusema kuwa anahitaji kuwa makini zaidi kumchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wake.


Haya ni maswali na majibu kama alivyopost Instagram.


“Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?
JIBU : Hatuja achana niliamua kumuacha
Kwanini umeachana/umemuacha mume?
JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa
Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo. .. ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo , sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii. Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume? JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshma zaidi kuishi na mume asie na heshma, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba.
Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini . Ukiachilia mbali vipigo.
Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao. …..niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso.
Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?
JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi
Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.
Kwanini usirudiane na mumeo?
JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpk kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. …
When i say never, I mean Never.
Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?
JIBU : Nilidhani angebadikika, so nilikuwa natoa nafasi.
Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.
Uliwezaje kuondoka?
JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu.
Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima km kweli ntaweza ku move on?
Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpk muda huu nnapo type na ku post haya majibu.
Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga.
Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.”

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani