UEFA CHAMPIONS :Matokeo ya Schalke na Real Madrid CF Ronaldo aibeba Real
MCHEZAJI
BORA Duniani Cristiano Ronaldo, ameiongoza Timu yake Real Madrid
kuifunga Schalke Bao 2-0 huko Gelsenkirchen katika Mechi ya Kwanza ya
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hadi
Mapumziko Real walikuwa mbele kwa Bao la Cristiano Ronaldo la Dakika ya
26 ambalo limemaliza ukame wake wa kutofunga katika Mechi 3 zilizopita
za Real.
Bao hilo
lilitokana na Krosi ya Fulbeki Carvajal aliyomimina kutoka Kulia na
Ronaldo kuunganisha kwa Kichwa na kumzidi maarifa Kipa Wellenreuther.
Real
walipiga Bao lao la Pili Dakika ya 79 kufuatia Ronaldo, akiwa Winga ya
Kushoto, kuwatambuka Mabeki wawili na kumlisha Marcelo alietumbukia
ndani ya Boksi na kuachia kigongo kwa Mguu wake ‘dhaifu’ wa Kulia na
kutingisha nyavu.
Marudiano ya Timu hizi ni huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid hapo Jumanne Machi 10 na Mshindi kutinga Robo Fainali.
VIKOSI:
SCHALKE: Wellenreuther; Uchida, Howedes, Matip, Nastasic, Aogo; Hoger (Meyer - 80'), Neustadter (Kirchhoff - 57'), Boateng; Choupo-Moting, Huntelaar (Platte - 33')
Akiba: Wetklo, Kirchhoff, Meyer, Fuchs, Ayhan, Barnetta, Platte.
REAL MADRID: Casillas; Carvajal (Arbeloa - 82'), Varane, Pepe, Marcelo; Lucas Silva, Kroos, Isco (Illarramendi - 85'); Bale, Benzema (Hernández - 78'), Ronaldo
Akiba: Navas, Hernandez, Arbeloa, Nacho, Jese, Illarramendi, Medran.
MATOKEO MENGINE
FC BASEL 1 FC PORTO 1
FC Basel na
FC porto zimetoka Sare ya Bao 1-1 huko Uswisi katika Mechi ya Kwanza ya
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mpaka Mapumziko FC Basel walikuwa mbele kwa Bao la Derlis Gonzalez la Dakika ya 11.
Porto
walisawazisha Dakika ya 48 kupitia Casemiro, Mchezaji wa Mkopo kutoka
Real Madrid, lakini Refa Mwingereza Mark Clattenburg alibadili uamuzi
wake baada ya Msaidizi wake kuashiria ni Ofsaidi.
Hata hivyo, Porto walisawazisha kwa Penati ya utata ya Dakika ya 79 iliyofungwa na Danilo Luiz da Silva.
Penati hiyo ilitolewa kufuatia Refa Clattenburg kuamua Clattenburg Walter Samuel kaunawa Mpira.
Marudiano ya Timu hizi ni huko Ureno hapo Jumanne Machi 10 na Mshindi kutinga Robo Fainali.
VIKOSI:
FC BASEL: Vaclik, Xhaka, Suchy, Samuel, Safari, Gonzalez (Callà - 25'), El-Nenny, Frei, Zuffi, Gashi Hamoudi - 83'), Streller (Embolo - 63')
Akiba: Vailati, Degen, Arlind Ajeti, Delgado, Hamoudi, Embolo, Calla.
FC PORTO: Fabiano, Danilo, Maicon, Marcano, Alex Sandro, Herrera, Casemiro, Torres (Neves - 68'), Tello Quintero - 81'), Martinez, Brahimi
Akiba: Helton, Martins Indi, Quaresma, Quintero, Evandro, Ruben Neves, Aboubakar.