Tundaman,Matonya Wamaliza ‘Bifu Lao
TZ MZUKA
08:15
0
Lile bifu la wasanii wa Bongo
Fleva,Tundaman na Matonya lililodumu kwa muda wa miaka nane limemalizwa
leo kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
Tundaman ndiye aliyekuwa wa kwanza
kuingia kwenye kipindi ambapo leo alikuwa akizungumza na mashabiki wake
na kuitambulisha ngoma yake mpya iitwayo ‘Achana na Mimi’ ambapo
mtangazaji wa kipindi hicho,Husna Abdul alimuuza kuhusiana na bifu na
Matonya alisema hana tatizo naye.
Ndipo Husna alipomuuliza kuwa kama
akitokea Matonya kwa muda huo anaweza kuongea naye na kupanishwa alisema
kuwa hata akitokea ataongea naye ingawa hajaonana naye tangu mwaka
2007.
Msanii Matonya alipigiwa simu na
kukutana na Tundaman kwenye kipindi na kupatanishwa bifu lao na kuondoka
pamoja kuelekea studio ambayo bado hawajaiweka wazi kufanya ngoma yao
ya pamoja.
Wasanii hao kwa vipindi tofautitofauti walikuwa wakituhumiana mambo mbaimbali huku Tundaman alishawahi kulalamika kuwa alimtungia Matonya wimbo wa Vaileth ambao ulifanya vizuri lakini msanii huyo hakuwahi kumshukuru wala kumtaja kwenye ‘interview’.