Home
»
Sports
»
FA CUP-FAINAL-ARSENAL vs ATON VILLA, NANI KUIBUKA BINGWA
TZ MZUKA
12:18
0
Jumamosi
Mei 30, Uwanjani Wembley, Jijini London kuanzia Saa 1 na Nusu Usiku,
Arsenal na Aston Villa zitagombea FA CUP kwenye Fainali na tayari
vijembe vishaanza kutembea.
Mchezaji wa Aston Villa, Ashley
Westwood, ameonya kuwa Wachezaji wa Arsenal hivi sasa hawapati usingizi
kwa kumwota Straika hatari wa Villa Christian Benteke.
Benteke
ni Straika wa Ubelgiji mwenye Miaka 24 na ameshapiga Bao 12 katika
Mechi zake 12 zilizopita baada ya kupona maumivu yake.
Westwood amesema: "Benteke sasa amerejea katika ubora wake. Arsenal hawatapenda kucheza nae."
Mwanzoni
mwa Msimu, chini ya Meneja alietimuliwa Paul Lambert, Benteke alififia
na kisha kuandamwa na Majeruhi lakini sasa chini ya Meneja mpya, Tim
Sherwood, Straika huyo ameibuka upya.
Lakini
Westwood ameonya pia kuwa Timu yao si Benteke peke yake kwani wanao
Fabian Delph, Tom Cleverly, Mchezaji wa Mkopo kutoka Man United, na
Chipukizi Jack Grealish mwenye Miaka 19 ambae aling'ara mno kwenye Nusu
Fainali ya FA CUP Villa ilipoibwaga LIverpool 2-1.
Tags :
Sports
Share !