Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » FULL TIME: CRYSTAL PALACE 1 vs 2 MANCHESTER UNITED, MAROUANE FELLAINI AIBEBA UNITED , AIPA BAO LA USHINDI UGENINI SELHURST PARK!


TZ MZUKA 02:05 0

2-1 Fellaini akisimamisha mashabiki Uwanjani baada ya kufunga bao la pili
Bao la Dakika ya 78 la Marouane Fellaini limewapa Manchester United ushindi wa Bao 2-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England waliyocheza Ugenini Selhurst Park na Crystal Palace.
Ushindi huu umewachimbia Man United kwenye Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 7 mbele ya Timu ya 5 Liverpool ambayo ndiyo pekee inaweza kuwang'oa Man United kwenye nafasi hiyo na kuwanyima kucheza UEFA msimu ujao.



Man United walitangulia kufunga katika Kipindi cha Kwanza katika Dakika ya 19 kwa Penati ya Juan Mata ambayo ilikuja baada ya Krosi ya Ashley Young kushikwa na Scott Dann.
Palace walisawazisha Dakika ya 57 kwa Frikiki ya Jason Puncheon iliyobabatiza mtu na kutinga lakini Krosi ya Ashley Young ilimfikia Fellaini aliefunga kwa Kichwa katika Dakika ya 78 na kuwapa Man United ushindi muhimu.
Ili kuhakikisha wanamaliza ndani ya 4 Bora bila kujali nini Liverpool wanafanya, Man United wanahitaji Pointi 3 tu katika Mechi zao mbili zilizobaki.
Man United wamebakisha Mechi moja Old Trafford na Arsenal na Ugenini na Hull City.
Lakini ikiwa Liverpool Jumapili watafungwa na Chelsea au kutoka Sare, njia ni nyeupe kwa Man United.
Fellaini akifanya yake dakika ya 78, akitupia kwa kichwa na kufanya 2-1Shabiki aliingia Uwanjani  baada ya Fellaini kusawazisha!Raha ya Ushindi bwaaanae!!!Chupchupuu!!!Marouane Fellaini aliifungia Manchester United bao la pili na kufanya 2-1 dakika ya 78 na mtanange kumalizika United wakiibuka kidedea kwenye Uwanja wa Selhurst Park, London mbele ya mashabiki 25009. Ushindi huu wa United unawapa Matumaini ya Kucheza Klabu Bingwa Ulaya msimu Ujao kwani wamefanikiwa kupata pointi 68 na wapo ndani nne bora wakiwa pia nafasi ya nne. Ashley Young akishangilia!Jason Puncheon dakika ya 57 kipindi cha pili alisawazisha bao na kufanya 1-1.Jason Puncheon akishangilia bao lake1-1Jason Puncheon baada ya kuweka sare
Juan Mata akichonga penati.Mpaka nyavuni!Mata akishangiliaPongezi kwa MataMchezo huu pia Umemalizika ukimwachia Majeraha Luke Shaw na kulazimika kuondolewa Uwanjani na huku Wayne Rooney akipumzishwa baada ya kuumia Mguu.Luke Shaw kaumia tena na Hapa ni Dokta akimcheki kwa karibu sanaLuke Shaw kaumia tena na kulazimika kuondolewa UwanjaniMeneja wa Newcastle United Alan Pardew alipata muda akateta na wachezaji wake na kuwapa mbinuLuke Shaw akiondolewa Uwanjani huko Ugenini Selhurst ParkRooney nae yale yale!Rooney alipumzishwa!
Wachezaji wa Crystal Palace wakimsimamia Mwamuzi Michael Olivier baada ya kutoa penati kwa UnitedJuan Mata dakika ya 19 kipindi cha kwanza aliifungia United bao kwa mkwaju wa penati nao Crystal Palace walisawazisha kupitia mpira wa adhabu frii kiki iliyofungwa na Jason Puncheon dakika ya 57 kipindi cha pili na kufanya 1-1.

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani