![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPdO9-W5p5PdT4BEwXvsvxxIu6vtf4lnMq9dOV64Sar9XEQ9Li4i4wWMACQO5oAd5D9nBd1uyhl3uAPCVpeeYwgLMXl2QiixVz7dbmSpSdhxTQJoJtXx10kTomN8ZLWVH_5CXWzZtrIV2P/s640/11242865_1616265461923409_742572034_n.jpg)
Mwanamke aliyekamatwa nyumbani kwa Chris Brown baada ya kuvunja na kufanya uharibifu, anaamini kuwa ni mke wa staa huyo.
Kabla ya hapo, Amira Kodcia Ayeb alipost
ujumbe mtandaoni kuwa yupo Malibu akitafuta nyumba yake. Msichana huyo
mwenye miaka 21 kutoka nchini Tunisia, anasema jina lake la mwisho ni
Brown.
Inawezekana anadhani kuwa Chris ni mume
wake na ndio maana aliandika “Mrs. Brown” kwenye magari ya staa huyo na
ndani ya nyumba yake. Rafiki wa Ayeb ameiambia TMZ kuwa Ayeb ni muimbaji
chipukizi anayesoma katika chuo kikuu cha Houston na alipanda basi wiki
iliyopita kwenda kumuona Chris.
Chris alimkuta msichana huyo kitandani kwake akiwa mtupu Jumatano hii na inadhaniwa alikaa ndani humo kwa siku mbili.
Kupitia Instagram, Chris alielezea mkasa huo:
I get home and find this crazy
individual in my house. She had broken the hinges off the doors. She
Found time to cook her several meAls. She Wrote “I love you” on the
walls. She threw out my daughters clothing as well as my dogs stuff.
Then had all these crazy voodoo things around my crib. goes to show you
how crazy people are crazy! And she painted her name on my cars!!!! I
love my fans but this is some on some real real crazy shit! I pray she
will get help .