Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» »Unlabelled » USAJILI BARANI ULAYA UKO HAPA


TZ MZUKA 22:49 0


DEFOE AJIUNGA NA SUNDERLAND
JERMAINE-DEFOEStraika wa Toronto FC na England, Jermain Defoe, amekamilisha upimwaji Afya yake akiwa njiani kuichezea Klabu ya Ligi Kuu England, Sunderland.
Meneja wa Sunderland, Gus Poyet, anataka kuimarisha ushambuliaji kwa vile wana tatizo kubwa la ufungaji Magoli.
Sunderland wapo Nafasi ya 16 kwenye Msimamo wa Ligi, wakiwa Pointi 1 juu ya Timu 3 za mkiani na wao ndio Timu ya pili nyuma ya Aston Villa kwa kufunga Bao chache kwenye Ligi wao wakiwa na Bao 18.
Defoe, mwenye Miaka 32, amekuwa akifanya Mazoezi na Timu yake ya zamani Tottenham baada ya Msimu wa MLS kumalizika huko Canada na Marekani kwenye Ligi ambayo Straika huyo amefunga Bao 11 katika Mechi 16 kwa Klabu yake Toronto FC katika Msimu wake wa kwanza.
Kwenye Ligi Kuu England, alipozichezea Klabu za West Ham, Tottenham na Portsmouth, Defoe alifunga Jumla ya Mabao 124 na kumfanya ashike Nafasi ya 14 katika Historia ya Ufungaji Bora wa Ligi Kuu England.
WILFRIED BONY RASMI MAN CITY
Manchester City wamekamilisha Uhamisho wa Straika wa Swansea City Wilfried Bony kwenye Dili itakayofikia Pauni Milioni 28.WILFRED-BONY
Bony amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Nusu na atakuwa huko Etihad hadi Mwaka 2019 akivaa Jezi Namba 14.
Akiongea baada ya kusaini Mkataba, Bony, ambae sasa yuko na Timu ya Taifa ya Ivory Coast kwa ajili ya AFCON 2015 itakayoanza huko Equatorial Guinea Jumamosi, alisema: “Najisikia vyema sana, ni heshima kubwa kuwa hapa na ni ni changamoto kubwa!”
Bony, mwenye Miaka 26, alijiunga na Swansea kwa Dau la Rekodi ya Klabu la Pauni Milioni 12 kutoka Vitesse Arnhem ya Uholanzi Mwaka 2013 na Mwaka 2014 ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England baada kupachika Bao 20.
Ada hii ya kumnunua Bony pia imevunja Rekodi ya Swansea ya kuuza Mchezaji ambayo ilikuwa ni Pauni Milioni 15 walipomuuza Joe Allen kwa Livepool hapo Agosti 2012.
Kwenye Uhamisho hu, Man City watalipa Pauni Milioni 25 kwa mkupuo na zilizobaki zitalipwa kulingana na Mechi atakazocheza Straika huyo.
Msimu huu Bony, ambae sasa yuko na Timu ya Taifa ya Ivory Coast kwa ajili ya AFCON 2015, ameifungia Swansea Bao 9 katika Mechi 22.
MAN UNITED YAMFUKUZA MSAKA VIPAJI
Torben-AakjaerManchester United imemfukuza mmoja wa Wasaka Vipaji wao kufuatia madai aliposti maneno ya Kibaguzi kwenye Mtandao wa Facebook.
Ripoti iliyochapishwa na Gazeti la Uingereza, Guardian, ilidai Torben Aakjaer, Raia wa Denmark, alichapisha maneno ya Kibaguzi kupinga Uhamiaji kwenye Facebook.
Mara baada ya tuhuma hizo kuibuka, Manchester United ilimsimamisha Torben Aakjaer na kisha kumfukuza baada ya uchunguzi wa muda mfupi.
Msemaji wa Man United alieleza: “Tumefuta uhusiano wetu na yeye [Aakjaer]. ”
Awali kabla kumfukuza, Man United ilitoa taarifa iliyomalizia: “Manchester United ni tassisi inayojumuisha wote na haitovumilia vitendo vya aina hii.”
Aakjaer alianza kazi na Man United Mwaka 2011 na kabla ya hapo alikuwa na Klabu ya Germany Hamburg.

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani