TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA ZIKO HAPA
TZ MZUKA
21:53
0

Lille wapo tayari kukubali ofa ya kiasi cha Euro milioni 3.5 kutoka kwa Liverpool ambacho kitamruhusu Divock Origi kwenda Anfield mwezi Januari lakini klabu hiyo ya Ufaransa inataka kumsajili mbadala wa raia huyo wa Ubelgiji kabla ya kukamilisha dili hilo.

Juventus wapo tayari kumsaini mshambuliaji wa Monaco,Radamel Falcao kama Manchester United watashindwa kulipa kiasi cha Euro milioni 45 ili kumpa mkataba wa kudumu ndani ya Old Trafford.

Meneja wa Manchester City,Manuel Pellegrini anataka kumnasa Julian Draxler. Schalke wanataka Matija Nastasic awe katika seemu ya dili hilo ili kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwenda Etihad.

Juventus wanataka kuhakikisha wanawazuia Paul Pogba kwa kumuwekea ada ya kiasi cha pauni milioni 70 huku wakitaka kuwaongeza Radamel Falcao, Ramires na Miranda katika kikosi chao.

Ripoti zinadai kwamba meneja wa Southampton,Ronaldo Koeman anamatumaini ya kumsaini Bruno Martins Indi kutoka Porto. Kocha huyo alisema ifikapo dirisha la usajili anatazamia kumsajili beki ambaye alicheza katika klabu ya Feyenoord.

Klabu ya Crystal Palace inajiandaa kupambana na QPR kwaajili ya kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa West Ham,Mauro Zarate.

Liverpool wapo tayari kupeleka ofa kwa mshambuliaji wa Valencia,Paco Alcacer. Chipukizi huyo ana kiasi cha pauni milioni 14.1 zaidi katika mkataba wake ambacho wekundu hao wapo tayari kukilipa.