Taarifa za Angel Di Maria kutaka kuondoka Manchester United..
TZ MZUKA
04:04
0
Mwenyewe ameibuka, anamtaka wakala wake ambaye anaitwa Jorge Mendes kumtafutia timu nyingine kwa ajili ya kwenda kucheza na yuko tayari kuondoka kwenye klabu hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
Klabu za Barcelona, PSG na Juventus zimeonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo ingawa hajafanya mazungumzo yoyote na klabu hizo mpaka sasa.
Kwa mujibu wake Di Maria amesema amechoka kuitumikia klabu hiyo na anatamani kuona akicheza sehemu nyingine.
Di Maria alisainiwa Man United mwaka 2014 akitokea Real Madrid na kukabidhiwa jezi namba 7 ambayo ni ya kishujaa kwenye klabu hiyo, imevaliwa na mastaa wa soka kama George Best, Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo.