Di Maria ajichora ‘Tattoo’ mpya namba saba 7
TZ MZUKA
02:55
0
Picha mpya imetawala kwenye
mitandao ya kijamii jumatatu hii ikimuonesha Di Maria akiwa na ‘tattoo’
mpya kwenye mkono wake wa kushoto.
Di Maria alikuwa tayari ameshajichora Tattoo kwenye mkono wake, lakini ameongeza namba 7 karibu na kiwiko chake.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real
Madrid anavaa jezi namba 7 Old Trafford na mashabiki wengi wamechukua
picha hiyo inayomaanisha yuko tayari kukaa kwa muda mrefu Man United.
Msimu wa kwanza wa Di Maria ligi kuu England umekuwa mgumnu baada ya kusajiliwa kwa paundi milioni 59.7 kutoka Real Madrid.
Di Maria amefunga magoli manne
(4) katika mechi 28 alizocheza Man United na amekuwa akihusishwa kuhamia
PSG kufuatia kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Old
Trafford.