LA LIGA: MESSI HETITRIKI, NEYMAR 1, SUAREZ 1, BARCA 5-0!
TZ MZUKA
10:18
0
Hii Leo Barcelona wakiwa kwao Nyumbani Nou Camp waliichapa Levante Bao 5-0, huku Lionel Messi akipiga Hetitriki, na kuwakaribia Vinara wa La Liga Real Madrid na sasa wapo Pointi 1 nyuma yao.
Hadi Mapumziko, Barca walikuwa mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao za Neymar, Dakika ya 17, na Lionel Messi, Dakika ya 38.
Kipindi cha Pili, Messi aliongeza Bao 2, moja la Penati, na Luis Suarez kupiga 1 na kuwatwanga Levante Bao 5-0.
VIKOSI:
Barcelona (Mfumo 4-3-3): Bravo; Montoya, Bartra, Mascherano, Adriano; Rakitic, Busquets, Xavi; Pedro, Messi, Neymar.REFA: Javier Estrada Fernández
Levante (Mfumo 4-2-3-1): Marino; Ivan Lopez, Navarro, Ramis, Tono; Simao, Diop; Xumetra, Barral, Morales, Uche.
REFA: Mario Melero López