UEFA Champions League;Matokeo ya Man City vs FC Barcelona
TZ MZUKA
14:12
0
Michuano ya ligi ya mabingwa wa ulaya imeendelea leo tena katika
hatua ya 16 bora ya michuano – ambapo mabingwa wa England, Manchester
City waliikaribisha FC Barcelona katika dimba la Eithad katika mchezo wa
raundi ya kwanza ya hatua hiyo ya mtoano wa michuano hiyo.
Barca ambao waliitoa City katika michuano hii msimu uliopita,
wamefanikiwa kuingiza mguu mmoja ndani kwenye hatua ya robo fainali
baada ya kupata ushindi wa 2-1.
Magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Luis Suarez katika dakika ya 16 na 30 ya mchezo.
Sergio Aguero aliifungia City goli la kufutia machozi katika dakika ya 69.
Mechi hiyo itarudiwa wiki mbili zijazo katika dimba la Camp Nou jijini Barcelona.
JUVENTUS VS BORUSSIA DORTMUND