MESSI AITENGENEZA BAYERN ,BARCA IKISHINDA 3-0
TZ MZUKA
21:47
0
Lionel Messi ameonyesha kweli anaweza, kweli
ni mchezaji wa “dunia” baada ya kufunga mabao mawili na kutengeneza moja na
kuiwezesha Barcelona kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Bayern Munich.
Katika mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali
ya Ligi ya Mabingwa, Messi amefunga mabao hayo mawili kwa uwezo binafsi wakati
Barcelona ilionekana imeshindwa kuupennya ukuta wa Bayern iliyokuwa ugenini.
Mabao hayo mawili yalionyesha kuwachanganya
mabingwa hao wa Ujerumani wanaofundishwa na Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep
Gaurdiola na kuwasababisha watoe bao la tatu lililofungwa kwa ulaini na Neymar.
Bayern wanalazimika kujipanga ili kushinda
zaidi ya mabao matatu katika mechi itakayopigwa mjini Munich.