Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » Manchester United yamsajili Mholanzi Huyu


TZ MZUKA 09:14 0

Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuwa imefikia makubaliano na viongozi wa klabu ya PSV Eindhoven ya kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uholanzi, Memphis Depay, itapofika mwishoni mwa msimu huu.


Magazeti ya De Telegraaf na Voetbal International, ya nchini Uholanzi yameripoti kwamba pande hizo mbili zimekubaliana kufanya makubaliano ya biashara ya usajili wa mshambuliaji huyo wa pembeni ambaye thamani yake ni Euro million 30 ni sawa na paundi milioni 22.3.
Depay1
Mitandao ya kijamii ya Twitter ya vilabu hivo viwili vya PSV na Man Utd imeandikwa taarifa hizo, ikiwa ni uthibitisho rasmi wa kuuzwa kwa Depay mwenye umri wa miaka 21.
Depay2
Depay, anaongoza kwa upachikaji wa mabao katika ligi ya nchini Uholanzi msimu huu kwa kufunga mabao 21. Mkataba wake wa kujiunga na Man Utd utakamilika mwezi ujao kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu utakaoenda hadi 2018.

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani