Sitti Mtemvu asimulia jinsi alivyoumizwa na uzushi kuwa ana uhusiano na baba yake mzazi
TZ MZUKA
02:08
0
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ajivue taji hilo mwaka jana aliyoyafanya live jana kwenye kipindi cha Nirvana cha EATV, mrembo huyo aliyezindua kitabu chake ‘Chozi la Sitti’ hivi karibuni, alifunguka mengi tusiyoyajua.
Sitti alisema aliamua kujivua taji hilo kwakuwa shutuma dhidi yake zilizokuwa zikiandikwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari, zilikuwa nzito kuzihimili.
“Hali ile ilikuwa inani-affect mimi pamoja na familia yangu,” alisema. “Sawa nilikuwa na dream ya kuwa miss lakini ikawa inaathiri familia yangu. Ndio maana nikaamua ‘OK acha nirudishe maneno yamekuwa mengi hata nikikaa nayo siwezi kuwa happy.”
Sitti alizikanusha tena tuhuma za kuwa na mtoto na kudai mtoto aliyekuwa akionyeshwa kwenye mitandano ni mdogo wake.
“Yule mtoto waliokuwa wanasema ni mtoto wangu ni mdogo wangu wa mwisho na watu wengi wanamjua nimekuwa nam-posti kwenye mitandao,” alisisitiza Sitti.
“Mdogo wangu aliumia sana. Ilifikia hatua alikuwa anaenda shule marafiki zake wanamtania kwa sababu sometimes naendaga kumchukua shule so wananijua. So ikafikia hatua marafiki zake wanamwambia ‘umetudanganya kumbe yule ni mama yako, wewe ni mtoto wa bibi bomba.’ Kwahiyo ilimuathiri ikafika wakati akawa hataki kwenda shule analia kwamba ‘sitaki kwenda shule wenzangu wananitania! Kuna siku moja nakumbuka alikuja nyumbani na mimi nilisimuliwa na mama, niliumia sana, kwamba ameona kitu kibaya wameandika kuhusu Sitti, baada ya kumbembeleza ndio akasema ‘nimeona kuna sehemu wameandika Sitti ni girlfriend wa baba!”
Katika hatua nyingine Sitti alisema hausiki na hajasababisha kufungiwa kwa shindano la Miss Tanzania.
“Sijui kama nahusika na sijui kama sihusiki, sijaona sehemu ambayo wameandika imefungwa Miss Tanzania sababu ya Sitti, kwamba nahusika? Hapana, kama nilivyokwambia sidhani kama nahusika vitu vingi vinaweza kutokea kwa wakati mmoja.” alisema Sitti.
Pia Sitti aliyegoma kuzungumzia umri wake, alizikanusha tetesi za kutoa rushwa ya ngono kwa mwaandaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
“Hakuna uhusiano wowote kati yangu na Hashim Lundenga na hayo maneno yaliandikwa mengi kusema mimi na mtoto, ni maneno ya watu ambao walijisikia kama kunichafua.”
Sitti amewataka wadau na mashabiki wake kukitafuta kitabu chake cha ‘Chozi la Sitti’ ambacho ndani kimezungumzia mambo mbalimbali kuhusu maisha yake pamoja na changamoto alizopitia.