Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » LIGI KUU ENGLAND: MAN UNITED YAIPIGA SPURS 3-0!


TZ MZUKA 15:28 0

Wakiwa kwao Uwanjani Old Trafford, Man United Leo hii wameonyesha dhamira yao thabiti ya kumaliza angalau 4 Bora ya Ligi Kuu England baada ya kuitwanga Tottenham Bao 3-0 ambazo zote zilifungwa Kipindi cha Kwanza.
Hadi Mapumziko Man United walikuwa mbele kwa Bao 3-0 kwa Bao za Marouane Fellaini alipokea Pasi Safi toka kwa Michael Carrick na kumalizia vizuri katika Dakika ya 9.
Kisha katika Dakika ya 19 Michael Carrick akafunga Bao la Pili kwa Kichwa baada ya Kona kuunganishwa kwa Kichwa na Fellaini na kuokolewa na Carrick kumalizia.
Dakika ya 34 Kepteni Wayne Rooney alipiga Bao la 3 alipounasa Mpira karibu ya Mstari wa Kati na kuwapita Mabeki wa Spurs Dier na Rose na kisha kumhadaa Kipa Hugo Lloris na kufunga.
Mara baada Mpira kutinga wavuni, Rooney alishangilia kwa kucheza Ngumi na kisha kujidondosha chini akivunga amepigwa Ngumi na kuzirai ikiwa ni jibu la habari zilizozagaa mitandaoni hii Leo kuwa alipigwa Ngumi na kuzirai Jikoni Nyumbani kwake wakati akifanya mzaha wa kucheza Ngumi na Mchezaji wa zamani wa Man United Phil Bardsley ambae sasa anacheza Stoke City.
Huko Goodison Park, Wenyeji Everton waliichapa Newcastle Bao 3-0 kwa Bao za Dakika ya 20 za John McCarthy, Penati ya Romelu Lukaku ya Dakika ya 56 na la 3 kwenye Dakika za Majeruhi kupitia Ross Barkley.
Newcastle walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao Fabricio Coloccini kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 59.
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea, Vakencia, Jones, Smalling, Blind, Herrera, Carrick, Mata, Fellaini, Young, Rooney
Akiba: Lindegaard, Rafael, Blackett, Pereira, Januzaj, Falcao, Wilson
TOTTENHAM: Lloris, Walker, Dier, Vertonghen, Rose, Bentaleb, Mason, Townsend, Eriksen, Chadli, Kane
Akiba:  Chiriches, Paulinho, Adebayor, Lamela, Vorm, Dembele, Davies
REFA: Mark Clattenburg


MATOKEO
Jumapili Machi 15
Chelsea 1 Southampton 1
Man United 3 Tottenham 0
Everton 3 Newcastle 0

 Credit To;;www.sokaintanzania.com

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani