JUVENTUS YAICHAPA MADRID BAO 2-1, TEVEZ SHUJAA
TZ MZUKA
14:14
0
Ingawa watu waliidharau Juventus,
lakini imeanza mechi yake ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
kwa kuwatuliza Real Madrid kwa kuwachapa 2-1.
Madrid ikiwa ugenini ilijikuta
ikifungwa bao kupitia Alvaro Morata kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Madrid.
Lakini shujaa wa Juventus alikuwa ni
Carlos Tevez aliyefunga bao la pili katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa
penalti.