Select Menu
Select Menu

Sports

Sports

Entertainment

Music

Video

News

Video

» » UCHAGUZI WA RAIS FIFA KUENDELEA LICHA MAAFISA 7 KUBAMBWA KWA RUSHWA!


TZ MZUKA 10:57 0

FIFA imesema Uchaguzi wa Rais wa Shirikisho hilo utaendelea Ijumaa licha ya Maafisa wao 7 kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya zaidi ya Dola 150 Milioni.
Ijumaa Kongresi ya FIFA inapiga Kura za Uchaguzi wa Rais ambapo Rais wa sasa, Sepp Blatter, anawania kiti hicho kwa mara ya 5 huku akikabiliwa na Mpinzani mmoja, Mwana wa Mfalme Ali bin al-Hussein kutoka Jordan.
Maafisa waliobambwa Leo kwa tuhuma za rushwa ni pamoja na Makamu wa Rais wa FIFA, Jeffrey Webb, na Eduardo Li, Julio Rocha, Costas Takkas, Eugenio Figueredo, Rafael Esquivel na Jose Maria Marin.
Maafisa wa Polisi wa Uswisi waliivamia Hoteli ya Baur au Lac Mjini Zurich ambayo Wajumbe wa FIFA wamefikia kwa ajili ya Uchaguzi wa Ijumaa na kuwanasa Maafisa hao 7 kutokana na Mashitaka yaliyofunguliwa na Idara ya Sheria ya Marekani ambayo imefungua Mashitaka 47 kwa Watuhumiwa 14 wanaodaiwa kuhusika na rushwa na utakatishaji Fedha kwa kipindi cha Miaka 24.

«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani